WANABLOGU NA WAANDISHI WA MITANDAO WAKUTANA NA MKURUGENZI WA MAWASILIANO IKULU

Mkurugenzi Wa Mawasiliano ya RAIS Ikulu,Bw.Bakati Machumu.

wanablogu na waandishi wa mitandao ya kijamii wamekitana na Mkurugenzi Mpya wa Mawasiliano Ikulu, Bw. Bakari Machumu, katika mkutano maalum wa utambulisho uliofanyika Ikulu 27 Novemba 2025.

Katika mkutano huo, Bw. Machumu aliwasilisha dhamira yake ya kujenga ushirikiano, uwazi, na mawasiliano bora kati ya Ikulu na wadau wa habari, hasa waandishi wa maudhui ya mtandaoni.
Hakukuwa na ajenda iliyofichwa, wala mpango wowote wa nyuma ya pazia.
Taarifa zinazotolewa kinyume na ukweli huu ni uzushi na hazifai kuaminiwa

 



Waandishi wa Habari wa Mtandaoni, pamoja na Wanablogu mbalimbali wakizungumza katika Kikao cha pamoja na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bw. Bakari Machumu, Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 27 Novemba, 2025.

Aidha TBN imesema inasikitishwa na kusambazwa kwa kipande kifupi cha video kutoka mkutano huo na baadhi ya watu, akiwemo wanasiasa, kwa lengo la kuchochea utata na kuibua tafsiri potofu kutoka kwenye kikao cha kawaida cha kiutendaji.

Ambapo wamesema wanasisitiza umuhimu wa mijadala yenye staha, maadili, na ukweli, kwani upotoshaji unadhoofisha tasnia ya habari na kupunguza uelewa sahihi ndani ya jamii.


Kiongozi Wa TBN Bwn.Beda Msimbe


TBN inatoa pongezi kwa Bw. Machumu kwa kujenga mazingira ya ushirikiano na wadau wote wa habari. Tunaamini kuwa uwazi, utulivu, na mawasiliano ya kuheshimiana ndiyo silaha muhimu zaidi dhidi ya taarifa potofu na uzushi.


Comments

Popular posts from this blog

KARNE YA AI: SADC BADO KUNA PENGO LA MAWASILIANO YA SAYANSI

MTANDAO WA WANABLOGU TANZANIA (TBN) WATOA UFAFANUZI KUHUSU MKUTANO WA IKULU

TUTAPONYA WAATHIRIKA WA MATUKIO YA OKTOBA 29, 2025