WANAOBEZA KAULI YA MSIGWA HAWAFAHAMU UWAJIBIKAJI WA VYOMBO VYA HABARI WAKATI WA MACHAFUKO.
Msigwa msemaji Mkuu Wa Serikali.
Pongezi za Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, kwa waandishi wa habari nchini kutokana na namna walivyotekeleza wajibu wao wakati wa vurugu za Oktoba 29, zimezua mijadala mikubwa katika mitandao ya kijamii. Wapo waliozipokea kwa mtazamo chanya na wapo wanaozihoji au kuzibeza.
Hata hivyo, uchambuzi wa kina unaonesha kwamba wanaozishambulia pongezi hizo mara nyingi hawatambui uzito, hatari, na dhamana kubwa ya vyombo vya habari wakati wa matukio ya sintofahamu.
Kwa hakika, katika nyakati za misukosuko, waandishi hawabebi kalamu tu hubeba ustawi wa taifa, amani ya jamii, na mara nyingi hutengeneza mazingira ya kuokoa nchi dhidi ya jazba.
Akizungumza kuhusu kauli ya Msigwa, mwandishi mkongwe na Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN), Beda Msimbe, alitoa mtazamo wa kitaalamu juu ya umuhimu wa pongezi hizo.
“ Waandishi waliokoa Amani Katika mazingira ya kawaida kabisa, Msemaji Mkuu alifanya vyema kutoa pongezi. Waandishi walionesha ukomavu, uzalendo na uwajibikaji mkubwa. Walitanguliza maslahi ya taifa kuliko ya binafsi au ya kisiasana hivyo kuzuia moto ambao ungeweza kuharibu nchi.”Alisema Beda Msimbe Mwenye kiti Wa TBN
Kwa maoni haya, inaonekana wazi kuwa pongezi hizo hazikulenga kubembeleza bali kutamka ukweli wa mchango muhimu uliofanywa na vyombo vya habari katika kipindi cha taharuki.
Jukumu Kubwa la Kijamii Kwa vyombo vya Habari Katika Wakati wa Machafuko ni:-
Kuzuia Uvumi Usio na Ukweli
Vyombo vya habari vina nguvu ya kuamsha au kupoza hasira za jamii. Katika machafuko, taarifa zisizo sahihi huweza kuchochea ghasia zaidi. Uwajibikaji wa waandishi ulihakikisha uvumi haukusambaa.
Kutokutumiwa kama Daraja la Ajenda Hasi.
Wanasiasa au makundi yenye nia ovu yanaweza kutumia habari vibaya. Ukomavu wa waandishi umeziba mianya ya ajenda hizi kufanikiwa.
Kuimarisha Utulivu Badala ya Kuchochea
Badala ya kuripoti kwa jazba, lugha chafu, au picha kali, waandishi walichagua njia ya kujenga utulivu, si kuangamiza.
Kulinda Msingi wa Taifa: Amani
Amani si jambo la kawaida ni matokeo ya maamuzi yenye busara. Vyombo vya habari vilichagua kuwa sehemu ya suluhisho, si chanzo cha tatizo.
Mafunzo na Nidhamu ya Kitaaluma Ndio Chanzo cha Mafanikio
Pongezi hizi zinatokana pia na mafunzo kadhaa ambayo waandishi hupitia, hasa kuelekea uchaguzi au matukio nyeti ya kitaifa. Mafunzo hayo huwakumbusha kuwa:
Kipaumbele ni utulivu wa nchi, si kutafuta views.
Mtangulizo wa habari haustahili kuongeza moto,Kipindi cha machafuko kinahitaji busara zaidi kuliko kasi ya kuchapisha taarifa.
Kwa kujali haya, walisaidia kuanza mapema hatua ya upatanishi na uponyaji wa taifa.Pongezi za Msigwa Ni Haki, Si Utata.
Kwa mtazamo wa kitaalamu, Msigwa hakufanya kosa kupongeza Badala yake, alionyesha kutambua kazi ngumu na ya kimkakati iliyotekelezwa na waandishi wa habari.
Waandishi hawakutafuta sifa, bali walifanya huduma ya kijamii ya kiwango cha juu kwa kuhakikisha Watanzania wanaendelea na shughuli za maisha bila taharuki.
Tunapaswa kufahamu kuwa pongezi hizo ni kwa ajili ya Kuimarisha misingi ya Amani,Kuhimiza Utaalamu,kuenzi Uzalendo na Kuimarisha Uwajibikaji katika tasnia ya habari
Waandishi Wamefanya Kazi Kuu, Taifa Linatambua Kazi ya waandishi wakati wa migogoro mara nyingi haipokei “likes” nyingi au sambaza mitandaoni Lakini wao ndio nguzo ya kile tunachokiita nchi tulivu.
Kupitia uamuzi wao wa kutanguliza nchi kuliko jazba, wameweka msingi imara wa kuendelea kulinda uhuru, demokrasia na utulivu wa Watanzania milioni 62.
#Msigwa#VyomboVyaHabari#MediaResponsibility#TanzaniaMedia#BreakingNewsTZ#Analysis#TBN#HabariZaLeo#Uchambuzi#AmaniYaTaifa
Comments
Post a Comment