Posts

TUTAPONYA WAATHIRIKA WA MATUKIO YA OKTOBA 29, 2025

Image
  Na Mwandishi Wetu  Jaji Mkuu mstaafu na Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya uvunjifu wa amani wakati na baada ya uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 Mohammed Chande Othman amesema katika kutekeleza wajibu wa Tume hiyo, wanatarajia kuponya waathirika wa vurugu hizo pamoja na watuhumiwa wa matukio hayo ya Oktoba 29. Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Disemba Mosi, 2025, Jaji Chande amesema watawatafuta walioshiriki, Vyama vya siasa, asasi za kiraia, wasimamizi wa uchaguzi na Tume huru ya Taifa ya uchaguzi, Viongozi wa dini na Watu wengine ili kuzungumza nao kuhusu matukio hayo. Aidha pia ameeleza kuwa watazungumza pia na wajasiriamali, wafanyabiashara, watu mashuhuri, mamlaka za serikali za mitaa katika maeneo yaliyoathirika, Vyombo vya ulinzi na usalama, wanahabari na sekta binafsi pamoja na washirika mbalimbali wa maendeleo.

KARNE YA AI: SADC BADO KUNA PENGO LA MAWASILIANO YA SAYANSI

Image
  Ulimwengu wa sayansi na teknolojia unasonga kwa kasi ya ajabu. Mataifa makubwa duniani yanawekeza kwenye ubunifu, utafiti wa kisayansi, na teknolojia za kisasa. Teknolojia kama akili unde, kilimo cha kisasa na tiba za kibunifu zaidi zinabadilisha maisha katika mataifa makubwa duniani. Karne ya akili unde [AI], roketi zinavuka anga, kuna uvumbuzi na gunduzi nyingi katika teknolojia mpya kwa kasi ambayo dunia haijawahi kushuhudia. Mataifa makubwa yanawekeza, yanashirikiana, na yanapasha habari za sayansi kwa umma wao kwa kasi.Lakini upande mwingine wa dunia, ndani ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika [SADC], bado kuna pengo kubwa katika mawasiliano ya sayansi. Watafiti wanagundua, Serikali zinafanya miradi, taasisi zinavumbua, lakini taarifa 'hazitembei' kwa kasi inayohitajika. Bado haziwafikii vema wananchi wake, hazijengi uelewa na hazifanyi sayansi kuwa sehemu ya maisha ya kila siku. Ndani ya SADC, bado kuna pengo kubwa kati ya maendeleo ya ki-sayansi na jinsi ambavyo t...

WANABLOGU NA WAANDISHI WA MITANDAO WAKUTANA NA MKURUGENZI WA MAWASILIANO IKULU

Image
Mkurugenzi Wa Mawasiliano ya RAIS Ikulu,Bw.Bakati Machumu. wanablogu na waandishi wa mitandao ya kijamii wamekitana na Mkurugenzi Mpya wa Mawasiliano Ikulu, Bw. Bakari Machumu, katika mkutano maalum wa utambulisho uliofanyika Ikulu 27 Novemba 2025. Katika mkutano huo, Bw. Machumu aliwasilisha dhamira yake ya kujenga ushirikiano, uwazi, na mawasiliano bora kati ya Ikulu na wadau wa habari, hasa waandishi wa maudhui ya mtandaoni. Hakukuwa na ajenda iliyofichwa, wala mpango wowote wa nyuma ya pazia. Taarifa zinazotolewa kinyume na ukweli huu ni uzushi na hazifai kuaminiwa   Waandishi wa Habari wa Mtandaoni, pamoja na Wanablogu mbalimbali wakizungumza katika Kikao cha pamoja na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bw. Bakari Machumu, Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 27 Novemba, 2025. Aidha TBN imesema inasikitishwa na kusambazwa kwa kipande kifupi cha video kutoka mkutano huo na baadhi ya watu, akiwemo wanasiasa, kwa lengo la kuchochea utata na kuibua tafsiri potofu kutoka kweny...

WANAOBEZA KAULI YA MSIGWA HAWAFAHAMU UWAJIBIKAJI WA VYOMBO VYA HABARI WAKATI WA MACHAFUKO.

Image
  Msigwa msemaji Mkuu Wa Serikali. Pongezi za   Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, kwa waandishi wa habari nchini kutokana na namna walivyotekeleza wajibu wao wakati wa vurugu za Oktoba 29, zimezua mijadala mikubwa katika mitandao ya kijamii. Wapo waliozipokea kwa mtazamo chanya na wapo wanaozihoji au kuzibeza. Hata hivyo, uchambuzi wa kina unaonesha kwamba wanaozishambulia pongezi hizo mara nyingi hawatambui uzito, hatari, na dhamana kubwa ya vyombo vya habari wakati wa matukio ya sintofahamu. Kwa hakika, katika nyakati za misukosuko, waandishi hawabebi kalamu tu hubeba ustawi wa taifa, amani ya jamii, na mara nyingi hutengeneza mazingira ya kuokoa nchi dhidi ya jazba. Akizungumza kuhusu kauli ya Msigwa, mwandishi mkongwe na Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN), Beda Msimbe, alitoa mtazamo wa kitaalamu juu ya umuhimu wa pongezi hizo.  “ Waandishi waliokoa Amani Katika mazingira ya kawaida kabisa, Msemaji Mkuu alifanya vyema kutoa pongezi. Waandishi wa...

MTANDAO WA WANABLOGU TANZANIA (TBN) WATOA UFAFANUZI KUHUSU MKUTANO WA IKULU

Image
  Mtandao wa Wanablogu Tanzania (TBN) Unatoa Ufafanuzi Kuhusu Mkutano wa Ikulu Dar es Salaam. Mtandao wa Wanablogu Tanzania (TBN) unapenda kutoa ufafanuzi rasmi na kuweka mambo wazi kufuatia taarifa zisizo sahihi na zinazoleta utata zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu mkutano uliofanyika hivi karibuni Ikulu. TBN inakanusha vikali madai yanayosambazwa na baadhi ya watu wanaojiita wanaharakati, wakidai—bila uthibitisho wowote—kuwa wanahabari wa maudhui ya mtandaoni waliitwa Ikulu jijini Dar es Salaam kwa lengo la "kupewa maelekezo" kuhusu maandamano yanayodaiwa kupangwa kufanyika tarehe 9 Desemba. Kusudi Halisi la Mkutano TBN inathibitisha kuwa madai haya si sahihi na yamekuwa yakipotoshwa. Kusudi la kweli na la moja kwa moja la wito wa Ikulu lilikuwa hili: Mkurugenzi mpya wa Mawasiliano Ikulu, Bw. Bakari Machumu, alifanya mkutano wa utambulisho rasmi na wadau muhimu wa sekta ya habari, akianza na wanahabari wa maudhui ya mtandaoni. Mkutano huu ulikuwa ni hatua muh...